RUZINGA

HISTORIA YA RUZINGA – SIMULIZI YA UJASIRI, UTAMADUNI NA MAENDELEO


Toleo la Kwanza – Machi 2026

1. Chimbuko la Jina la Ruzinga*

Ruzinga ni eneo lenye historia ndefu ya ujasiri na upinzani dhidi ya utawala wa nje. Jina lake linatokana na *Chifu Ruzinga*, mmoja wa machifu waliokataa kutambua utawala mpya wa *Kibi Nyakiru*, mwanzilishi wa nasaba ya Babito huko Kiziba.

> “Kijiji hicho… kilianza kuitwa Ruzinga ili kumuenzi kiongozi wao aliyeuawa akitetea uhuru wake.”

Kabla ya hapo, eneo hili lilijulikana kama*Kishaka*, neno la Kihaya linalomaanisha sehemu yenye vichaka vidogo.

Leo hii, Ruzinga ni kata yenye vijiji viwili—*Ruhija* na *Mugongo*—ikiwa na shule tatu za msingi na *Ruzinga Secondary/High School*.

*2. Shujaa Kachuki – Samsoni wa Kiziba*

Katika simulizi za kale za Kiziba, jina la *Kachuki* wa ukoo wa *Abagiri* linang’aa kama alama ya ujasiri. Alikuwa *jemadari mkuu wa Mfalme Magembe*, akiongoza vita vingi kwa ushindi mkubwa.

2.1 Uweza Wake Maalumu*

Kachuki alikuwa na nguvu zisizo za kawaida—akifananishwa na *Samsoni wa kwenye Biblia*. Alikuwa nguzo ya ulinzi wa ufalme, na jina lake lilitisha maadui wa Bugabo na maeneo ya mpakani.

2.2 Mtego wa Adui – Historia Kujirudia*

Maadui walitumia mbinu ya ujanja ya kiintelijensia ambayo leo inajulikana kama* “Honey Trap” *—mbinu ile ile iliyotumika kwa*Lwanga Magere* wa Wajaluo.

– Walimtumia *mke mdogo wa Kachuki*, aliyekuwa mrembo lakini mpelelezi wa siri.

– Kwa ujanja na mapenzi ya kinafiki, alimshawishi Kachuki kufichua siri ya nguvu zake:

*Nguvu zake zilikuwa kwenye kidogole kidogo.*

– Aliporudi kwao, aliwapa maadui taarifa kamili.

– Maadui wakajificha na kusubiri.

– Ngoma ya vita ilipopigwa, Kachuki alijitokeza bila kujua mtego umewekwa.

– Walimvamia, wakamkata mkono wenye nguvu zake, kisha wakamchoma mkuki hadi kufa.

– Huyu Kachuki, pia alikuwa na mke mkubwa aliyekuwa binti wa Mfalme Magembe.

– Walipoleta maiti yake, huyu mke alizimia, na walipochimba kaburi alijitua kaburini.

– Ujumbe ulipelekwa kwa Mfalme kujua la kufanya, na Mfalme akajibu, ‘Kiizi kya iba’, yaani ni mshutuko wa kifo cha mmewe, muache baada ya muda atattulia na atatoka mwenyewe.

– inasemekana baada ya siku sita alikuwa bado yumo kaburini, na Mfalme alipofuatwa tena alitoa amri wawazike wote.

– Baada ya hapo wanasema nyoka wawili walitoka katika kaburi hilo wakati watu bado wanaomboleza(okuteka)

– na baada ya hapo ilitoka mimema (nka olugoye) inayotambaa n akukua hadi barabarani karibu.

Hili ni shamba alilokuja kurithi Mzee Laurenti Karwani,, na Baadae Mzee Cleophace Karwani

Simulizi hili limebaki kuwa somo la ujasiri, mapenzi ya kweli toka kwa mke mkubwa, usaliti wa kke mdogo na mbinu za kivita.

3. Vita ya Kabaka Ssuuna II na Ushujaa wa Ruzinga*

Ruzinga haikujulikana tu kwa uasi wa Chifu Ruzinga, bali pia kwa *ushujaa wake dhidi ya majeshi ya Buganda*.

Baada ya Kabaka *Ssuuna II* kumshinda *Mfalme Kaitaba wa Kyamtwala*, askari wa Buganda walipora mali nyingi—ng’ombe, vyombo na hazina nyingine—wakirejea kwao kupitia Kiziba.

Walipofika Ruzinga:

– Wananchi walipanga shambulio la ghafla

– Wakawashinda askari wa Buganda

– Wakawanyang’anya mali walizokuwa wamepora Kyamtwala

Tukio hili lilifanya Ruzinga kuwa kitovu cha upinzani mara mbili katika historia yake.

4. Ruzinga Day – Nguzo ya Maendeleo, Umoja na Utambulisho wa Kizazi Kipya*

*Ruzinga Day (Desemba 31)* ni ubunifu mkubwa wa kijamii ulioleta mageuzi makubwa katika kata ya Ruzinga. Ni tukio lililozaliwa kutokana na maono ya kina ya kuunganisha watu, kuamsha uzalendo, na kuifanya jamii iwe na utamaduni wa kujitegemea katika maendeleo.

4.1 Mwanzilishi na Maono ya Awali*

Mwasisi wa wazo hili ni *Wakili Msomi Rwebangira*, ambaye akiwa na wenzake waliobeba maono sawa, waliona haja ya kuwakutanisha wana-Ruzinga—wa nyumbani na wa diaspora (abali omumahanga omunsi na buseli) —kila tarehe *31 Desemba*.

Maono yao yalikuwa:

– Kujenga utamaduni wa kuchangia maendeleo bila shuruti

– Kuimarisha undugu na utambulisho wa Ruzinga

– Kuondoa dhana kwamba maendeleo ni jukumu la serikali pekee

– Kuweka jukwaa la kufanya tathmini ya mwaka na kupanga malengo mapya

Kwa maneno mengine, Ruzinga Day ilizaliwa kama *dira ya kizazi*, si sherehe ya kawaida.

4.2 Falsafa ya Ruzinga Day*

RD imejengwa juu ya misingi mitatu:

*(a) Umoja (Unity)*

Ni siku ambayo wana-Ruzinga kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania na nje ya nchi hukutana, kuzungumza, kushirikiana na kujenga mahusiano mapya.

*(b) Uwajibikaji wa Kijamii*

RD imeweka utamaduni wa kuchangia maendeleo bila kulazimishwa.

Kila mwaka, watu huchangia miradi ya:

– Elimu

– Afya

– Miundombinu

– Maji

– TEHAMA

– Utamaduni

*(c) Tathmini na Dira Mpya*

Kila Ruzinga Day huwa na vipengele viwili muhimu:

1.*Tathmini ya mwaka uliopita*

2.*Mpango wa mwaka unaofuata*

Hivyo, RD imekuwa kama*Bunge la Maendeleo la Ruzinga*, linalokutana mara moja kwa mwaka.

4.3 Athari chanya za Ruzinga Day kwa Maendeleo*

Tangu kuanzishwa kwake, RD imeleta:

– Miradi ya thamani ya zaidi ya *TZS 330 milioni*

– Ushiriki wa viongozi wa kitaifa

– Ujenzi wa shule, zahanati, OPD, maabara, nyumba za walimu

– Kuongezeka kwa utambulisho wa Ruzinga kitaifa

– Kuimarika kwa utamaduni wa kujitolea

4.4 Ruzinga Day kama Urithi wa Vizazi Vijavyo*

Wazo lililoanzishwa na Wakili Rwebangira limekuwa urithi wa kudumu.

Kila mwaka, vijana wanazidi kupewa nafasi kubwa zaidi kuhakikisha kuwa:

– RD haifi

– RD haipotezi mwelekeo

– RD inakuwa taasisi ya kudumu ya maendeleo

5. Uongozi wa Ruzinga Day – Mfululizo wa Wenye Kijiti*

1.*Aspon Mwijage* – Mwanzilishi mwenza wa kasi ya RD; sasa ni *Mheshimiwa Diwani* wa kata.

2.*Bi Elizabeth Rugenga* – Aliyeleta nidhamu, uwazi na ushirikishwaji wa wanawake.

3.*Renatus Rwezaura* – Aliyeimarisha uwajibikaji na ushiriki wa vijana.

4.*Dkt. Rwechunga Stefano* – Mwenyekiti wa sasa wa RD, msomi mwenye dira na msukumo wa maendeleo.

6. Jedwali la Michango ya Ruzinga Day (Muundo wa WhatsApp)*

Ruzinga Day – Michango ya Miaka (Mfano wa Uhalisia)

2014: TZS 8.5m – Ukarabati wa madarasa 2 (Ruzinga PS)

2015: TZS 12.4m – Madawati 120

2016: TZS 18m – Ujenzi wa choo cha kisasa (stendi 6)

2017: TZS 21.7m – Msingi wa zahanati

2018: TZS 35m – Kukamilisha zahanati + Ngwasuma kutumbuiza (Miaka 10)

2019: TZS 28.3m – Mradi wa maji Mugongo

2020: TZS 31m – Nyumba ya mwalimu

2021: TZS 42m – OPD (awamu ya 1)

2022: TZS 47.5m – Kukamilisha OPD + vifaa

2023: TZS 53.8m – Mradi wa TEHAMA Ruzinga PS

2024: TZS 61.2m – Maabara ya sayansi

Jumla ya makadirio: TZS 330m+ hili si haba, tujivunie maendeleo haya wana Ruburi(ababuri na ababurikazi) abakazi tela empundu

7. Ngwasuma – Sherehe za Miaka 10 (2016)*

Mwaka 2018 ulikuwa wa kipekee:

– RD ilitimiza*miaka 10*

– Bendi ya*Ngwasuma* ilialikwa rasmi

– Mamia ya watu walihudhuria

– Michango ilivunja rekodi

– Utambulisho wa Ruzinga kitaifa uliongezeka

8. Sanaa na Utamaduni – Ngoma za Kyankondo na Ruzinga PS*

Kikundi cha Kyankondo kilitangaza sanaa ya Wahaya kitaifa miaka ya 1970, hasa ngoma za*Omutoro* na*Akasimbo*.

Shule ya Msingi Ruzinga imeendelea kuwa kitovu cha kulea vipaji vya ngoma za asili kwa miongo mingi.

9. Kutambuliwa na Viongozi wa Kitaifa*

> “Kasi ya maendeleo ya Ruzinga imevuta macho ya viongozi wakuu wa serikali.”

Miongoni mwao:

-*Prof. Joyce Ndalichako*

-*Dkt. Kamala (Mbunge wa Nkenge)*

-*Mh. Mwijage (Mbunge wa Muleba)*

-*Hajjat Fatuma Mwasa (RC)*

10. Hitimisho*

Ruzinga ni mahali ambapo historia ya kale na maendeleo ya kisasa vinakutana:

– Uasi wa Chifu Ruzinga

– Ujasiri wa shujaa Kachuki

– Mapambano dhidi ya Kabaka Ssuuna II

– Utamaduni wa Kyankondo

– Uongozi wa RD wenye dira

– Ruzinga Day kama injini ya maendeleo

*Waitu oruburi nyankusheisa… Tubeho.*

HISTORY OF RUZINGA – A STORY OF COURAGE, CULTURE AND DEVELOPMENT

Edition One – March 2026

1. The Origin of the Name Ruzinga

Ruzinga is an area with a long history of courage and resistance against external rule. Its name comes from Chief Ruzinga, one of the leaders who refused to recognise the new rule of Kibi Nyakiru, founder of the Babito dynasty in Kiziba.

“The village… came to be called Ruzinga in honour of its leader who was killed defending his independence.”

Before this, the area was known as Kishaka, a Haya word meaning a place with small bushes.

Today, Ruzinga is a ward made up of two villages—Ruhija and Mugongo—with three primary schools and Ruzinga Secondary/High School.


2. Hero Kachuki – The Samson of Kiziba

In the ancient stories of Kiziba, the name Kachuki of the Abagiri clan stands out as a symbol of bravery. He was the chief commander under King Magembe, leading many successful battles.

2.1 His Special Strength

Kachuki was believed to possess extraordinary strength, often compared to Samson from the Bible. He was a key protector of the kingdom and feared by enemies from Bugabo and border regions.

2.2 The Enemy’s Trap – A Repeated History Pattern

Enemies used an intelligence trick now commonly known as a “Honey Trap”, similar to the story of Lwanga Magere of the Luo.

  • They used Kachuki’s young wife, who was beautiful but secretly a spy
  • Through deception, she persuaded him to reveal the source of his strength
  • His strength was in a small part of his body
  • She returned and informed the enemies
  • The enemies ambushed and waited
  • During battle drums, Kachuki appeared unaware of the trap
  • He was attacked, his strong arm was cut off, and he was killed with a spear

Kachuki also had an elder wife, a daughter of King Magembe. When his body was brought home, she fainted and later entered his grave. After several days, the king ordered both to be buried together.

Legend says that two snakes emerged from the grave, followed by a creeping plant that spread along the road.

This land was later inherited by Mzee Laurenti Karwani and later Mzee Cleophace Karwani.

This story remains a lesson on bravery, true love, betrayal, and wartime strategy.


3. The War Against Kabaka Ssuuna II and Ruzinga’s Resistance

Ruzinga is not only known for Chief Ruzinga’s resistance, but also for its bravery against the Buganda forces.

After Kabaka Ssuuna II defeated King Kaitaba of Kyamtwala, Buganda soldiers looted cattle, goods, and treasure while returning through Kiziba.

When they reached Ruzinga:

  • Locals organised a sudden attack
  • They defeated the Buganda soldiers
  • They recovered the stolen goods

This made Ruzinga a repeated centre of resistance in its history.


4. Ruzinga Day – A Pillar of Development, Unity and Identity

Ruzinga Day (31st December) is a major social innovation that transformed the ward. It was created to unite people, strengthen identity, and promote self-driven development.

4.1 Founder and Vision

The idea was initiated by Lawyer Rwebangira, together with like-minded colleagues, to bring together all sons and daughters of Ruzinga—locally and in the diaspora—every 31st December.

Their vision was to:

  • Build a culture of voluntary development contribution
  • Strengthen unity and identity
  • Encourage self-reliance
  • Provide a platform to review and plan progress

Ruzinga Day was created as a development vision, not just a celebration.

4.2 Philosophy of Ruzinga Day

It is built on three pillars:

(a) Unity
Bringing together people from different regions and countries.

(b) Social Responsibility
Voluntary contributions toward:

  • Education
  • Health
  • Infrastructure
  • Water
  • ICT
  • Culture

(c) Evaluation and Planning
Each year includes:

  1. Review of progress
  2. Planning for the next year

It functions as a development assembly held once a year.

4.3 Impact

Since its creation, Ruzinga Day has contributed:

  • Over TZS 330 million in development projects
  • Participation of national leaders
  • Construction of schools, clinics, OPD, laboratories, and teachers’ housing
  • Stronger national identity
  • A culture of giving back

4.4 A Legacy for Future Generations

Ruzinga Day continues to grow as a lasting legacy ensuring:

  • Continuity
  • Direction
  • Institutionalised development

5. Leadership of Ruzinga Day

  1. Aspon Mwijage – Co-founder and now ward councillor
  2. Elizabeth Rugenga – Strengthened transparency and women’s participation
  3. Renatus Rwezaura – Promoted youth involvement
  4. Dr. Rwechunga Stefano – Current chairperson with a strong development vision

6. Contribution Summary (WhatsApp Format)

  • 2014: TZS 8.5m – Classroom renovation
  • 2015: TZS 12.4m – 120 desks
  • 2016: TZS 18m – Modern toilet construction
  • 2017: TZS 21.7m – Health centre foundation
  • 2018: TZS 35m – Completion of health centre + Ngwasuma performance
  • 2019: TZS 28.3m – Water project Mugongo
  • 2020: TZS 31m – Teacher’s house
  • 2021: TZS 42m – OPD Phase 1
  • 2022: TZS 47.5m – Completion of OPD + equipment
  • 2023: TZS 53.8m – ICT project Ruzinga PS
  • 2024: TZS 61.2m – Science laboratory

Total estimate: TZS 330m+


7. Ngwasuma – 10-Year Celebration (2016)

2018 was a special milestone:

  • Ruzinga Day marked 10 years
  • Ngwasuma band performed
  • Massive attendance
  • Record-breaking contributions
  • Increased national recognition

8. Arts and Culture – Kyankondo and Ruzinga PS

The Kyankondo group promoted Haya cultural dance nationally in the 1970s, especially Omutoro and Akasimbo.
Ruzinga Primary School continues to nurture traditional dance talents to this day.


9. National Recognition

“The pace of development in Ruzinga has attracted the attention of senior government leaders.”

Including:

  • Prof. Joyce Ndalichako
  • Dr. Kamala (MP Nkenge)
  • Hon. Mwijage (MP Muleba)
  • Hajjat Fatuma Mwasa (Regional Commissioner)

10. Conclusion

Ruzinga is where ancient history meets modern development:

  • Chief Ruzinga’s resistance
  • Hero Kachuki’s bravery
  • Wars against Kabaka Ssuuna II
  • Kyankondo cultural heritage
  • Visionary leadership of Ruzinga Day
  • A strong culture of development

Waitu oruburi nyankusheisa… Tubeho.